Muuguzi apata nafuu maambukizo ya Ebola

Image caption Muuguzi aliyepata maambukizo ya Ebola

Muuguzi kutoka Scotland aliyeugua virusi vya Ebola amepata nafuu.

Pauline Cafferkey alinusurika kupata virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola akifanya kazi nchini Sierra Leone, lakini baadaye akaja kuugua.

Baada ya kupata nafuu sasa ameondolewa katika hospitali moja huko London, alikokuwa ametengwa ili kupata matibabu ya ugonjwa wa utando wa Ubongo- yaani Menengitis, uliosababishwa na Ebola.