Marekani yamsaka Jihadi John

Haki miliki ya picha .
Image caption Jihadi John

Jeshi la Marekani limefanya uvamizi wa anga, kumkamata mpiganaji wa kundi la kigaidi la Islamic state ajulikanaye kama Jihadi John

Mohamed Emwanzi raia wa Uingereza ambaye alionekana kwenye video kadhaa akiua mateka ukingo wa magharibi.

Uvamizi huo uliofanyika jana karibu na mji wa Raqqa ulioko nchini Syria.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani -Pentagon- anasema wanafuatilia matokeo ya zoezi hilo kama liliweza kumuua Jihad John.