Moja kwa Moja: Mashambulio Paris

Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi

05.51:Pasipoti ya Misri na ile ya Syria zilipatikana katika miili ya washambuliaji wawili katika uwanja wa Stade de France ,kulingana na gazeti la Ufaransa La Liberation.

Kama ilivyoripotiwa hapo awali,maafisa wa polisi wa Ufaransa wanasema kuwa mmoja ya wavamizi katika eneo la Bataclan ametambulika kupitia alama za vidole vyake kama raia wa Ufaransa anayejulikana na vikosi vya usalama.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wanaweka maua katika eneo la uvamizi mjini Paris

05.41:Chombo cha habari nchini Ufaransa AFP kimeripoti kwamba raia wa Ufaransa ametambulika kama miongoni mwa washambuliaji wa ukumbi wa muziki mjini Paris.

Awali ripoti katika vyombo vya habari nchini Ufaransa,zilisema kuwa raia mmoja wa Ufaransa alibainika kupitia alama za vidole kama mtu anayejulikana na vikosi vya usalama ijapokuwa haijabainika iwapo ripoti hizo zinahusishwa na mshambuliaji huyo huyo.

05.18:Waziri wa maswala ya ndani nchini Ufaransa Bernard Cazenueve ameziagiza serikali za mitaani kuweka amri ya kutotoka nje iwapo zitahitajika kufuatia shambulio la mjini Paris.

Katika hotuba kwa runinga,Cazeneuve amethibitisha kwamba maafisa wa polisi wamepiga marufuku maandamano ya uma hadi siku ya Alhamisi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa usalama wakipiga doria mjini Paris

04.10:Maafisa wa polisi wamethibitisha kwamba wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuangusha mfuko katika uwanja wa ndege wa Gatwick.

Wataalam wameitwa katika uwanja wa ndege ili kuuchunguza mfuko huo.

Watu wameondolewa katika eneo la kupandia ndege huku baadhi ya safari za ndege zikicheleweshwa.

Image caption David Cameron

04.02:Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ametoa taarifa huko Downing stree akisema kuwa akisema kuwa tisho kutoka kwa kundi la wapiganaji la islamic state linabadilika na kuwa na lengo.

Sisi huku Uingereza tunakabiliwa na tisho kama hilo,''alisema.

Tutaongeza juhudi zetu maradufu ili kuangamiza itikadi hiyo.

3.25:Pasipoti ya Syria imepatikana katika mwili wa mmoja wa washambuliaji kulingana na chombo cha habari cha AP.Runinga ya Ufaransa pia imetoa habari hiyo ijapokuwa haijathibitishwa na BBC.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Francois Hollande

3.03:Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameelezea mashambulio yaliyotokea mjini Paris jana usiku na kuuwa watu kama 127 kuwa kitendo cha vita vilivyotangazwa na magaidi wa Islamic State.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kundi la islamic state limekiri kutekeleza shambulizi la Paris

02.11:Kundi la kigaidi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi la Paris.

01.56:Watu wameondolewa katika uwanja wa ndege wa Gatwick mjini London.Maafisa wa polisi wameiambia BBC kwamba wanakabiliana na 'kitu kinachotuhumiwa'.

Image caption Uwanja wa ndege wa Gatwick,London

12.29:Uchunguzi unaendelea kuhusu shambulizi la mjini Paris

Image caption Uchunguzi mjini Paris

12.19:Viongozi wa mashtaka mjini Paris wametoa idadi ya watu waliofariki kufikia 128 huku wengine 99 wakiwa na majeraha mabaya ,kulingana na ripoti za Reuters.

Image caption Rais Hollande

12.00:Wanajeshi wengine 1500 wametumwa kulinda jengo la bunge la Paris,maeneo ya kidini na vivutio vya utalii.Shule na vyuo vikuu vingi ambavyo hufunguliwa siku ya jumamosi vimefungwa ikiwa ni miongoni mwa hatua za usalama za dharura mjini humo.

11.59:Rais wa Ufaransa Francois Hollande kwa sasa anafanya mkutano wa usalama wa dharura na mawaziri pamoja na wakuu wa majeshi.

Image caption Paris

10:35 Makao makuu ya Kanisa Katoliki Vatican yametoa taarifa yakitaja mashambulio ya Paris kuwa "shambulio dhidi ya binadamu wote".

"Tunalaani (mashambulio haya) pamoja na Papa na watu wote wapenda amani," msemaji wa Vatican Federico Lombardi amesema kupitia taarifa.

10:29 Picha hii ya amani Paris yenye mchoro wa mnara wa Eiffel imekuwa ikisambazwa sana mtandaoni watu wakiwafariji watu wa Ufaransa.Mchoro huu umetoka kwa Jean Jullien.

Haki miliki ya picha Other

Image caption Paris

09:40 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameungana na viongozi wengine kushutumu uvamizi mjini Paris, na kusema mashambulio kama hayo lazima yakabiliwe kwa hatua kali. Ameahidi kutoa usaidizi na kuendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi.

09:30 Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alitisha mkutano maalum wa dharura wa baraza la mawaziri, ujulikanao kama Cobra, Downing Street kufuatia mashambulio nchini Ufaransa. Awali, alieleza kushtushwa kwake na mashambulio hayo yaliyoua watu zaidi ya 120.

09:20 Viongozi mbalimbali wameendelea kutoa risala zao

Waziri mkuu mpya wa Canada Justin Trudeau amesema wako pamoja na “binamu zetu Wafaransa wakati huu wa giza na majonzi”. Ameahidi kuisaidia serikali ya Ufaransa.

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ameshtushwa sana na “habari na picha zinazotufikia kutoka Paris”. Amesema anaomboleza na waathiriwa wa “linalodhihirika kuwa shambulio la kigaidi”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu mashambulio yaliyotekelezwa mjini Paris. Msemaji wa UN Stephane Dujarric amesema Ban ''anaamini Ufaransa ina uwezo wa kuwakamata na kuwatendea haki wahusika upesi."

09:12 Rais wa Iran Hassan Rouhani, aliyepangiwa kuzuru mji wa Roma na kisha Paris wikendi hii, ameahirisha ziara yake kutokana na mashambulio Paris.

07:50 Maafisa wa polisi wakisaidiana na wanajeshi wanashika doria maeneo mengi Paris baada ya watu 120 kuuawa katika mashambulio sita mjini humo. Hapa ni afisa wa polisi karibu na hospitali ya Saint Antoine mjini humo.

Haki miliki ya picha EAP

07:06 Raia wawili wa Sweden huenda wakawa miongoni mwa waathiriwa wa mashambulio Paris, wizara ya mashauri ya kigeni nchini humo imesema. Msemaji wa wizara hiyo Johan Tegel amesema wana habari raia mmoja wa Sweden amejeruhiwa na mwingine kuuawa.

07:00 Washambuliaji wanane wamefariki, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. Saba walijilipua, na mmoja akauawa. Wanne walifariki katika ukumbi wa Bataclan, watatu kwa kujilipua na mmoja akauawa na polisi.

Watatu walifariki karibu na uwanja wa michezo wa taifa naye wa nne akauawa barabarani mashariki mwa Paris.

06:24 'Ombeeni Paris' linasema bango hili lililoinuliwa na mwanafunzi kabla ya mechi kati ya Notre Dame Fighting Irish na St Francis Red Flash uwanja wa Purcell Pavillion mjini South Bend, Marekani. Hii ni baada ya mashambulio kuua watu zaidi ya 120.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu maeneo mengi duniani wameeleza kusikitishwa kwao na mashambulio yaliyotekelezwa Paris

06:21 Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa watu 200 wamejeruhiwa kwenye mashambulio yaliyotekelezwa Paris, 80 wamejeruhiwa vibaya

Haki miliki ya picha Getty

06:12 Gazeti la Le Parisien limeandika 'Cette fois, c'est la guerre' maana yake 'Wakati huu, ni vita'.

Limechapisha takwimu za waathiriwa wa mashambulio Ufaransa, ambazo linasema limepata kutoka kwa maafisa wa polisi.

Takwimu hizo ni kama ifuatavyo:

 • Bataclan: watu 100 wamefariki, saba wamo hali mahututi, wengine wanne wanauguza majeraha
 • Rue Charonne: 19 wamefariki, 13 hali mahututi, 10 wana majeraha
 • Rue Bichat: 14 wamefariki, 10 wamo hali mahututi, 10 wengine wamejeruhiwa
 • Avenue de la Republique: Wanne wamefariki, 11 wamo hali mahututi, 10 wengine wamejeruhiwa
 • Stade de France: Wanne wamefariki, 11 wamo hali mahututi, wengine 39 wamejeruhiwa
 • Rue Beaumarchais: watatu wamo hali mahututi, wanne wengine wanauguza majeraha

05:59 Shirika la habari la Associated Press limewanukuu polisi Paris wakisema wanaamini washambuliaji wote wameuawa. Kwenye shambulio la Bataclan, ambako watu 100 wanahofiwa kufariki, washambuliaji wanne walifariki.

05:35 Magazeti duniani yalivyoripoti habari za mashambulio yaliyotokea Paris na kuua zaidi ya watu 120

Haki miliki ya picha Other

05:25 Miji mingine duniani imeimarisha usalama baada ya mashambulio kutokea Paris. Hawa, ni maafisa wa polisi jijini New York

Haki miliki ya picha

05:24 Mghahawa wa Cafe la Bonne Biere ni mojawapo ya maeneo yaliyoshambuliwa. Hivi ndivyo hali ilivyo kwa sasa

Haki miliki ya picha AFP

05:22 Walionusurika wakumbatiana

Haki miliki ya picha Reuters

05:20 Polisi nchini Ufaransa wanasema washambuliaji wanne walifariki katika ukumbi wa Bataclan, watatu kati yao wakijilipua.

Haki miliki ya picha

04: 40 Maafisa wa serikali ya Ubelgiji wameambia shirika la habari la AFP kwamba usalama umeimarishwa na hasa kwenye mpaka wake na Ufaransa kufuatia mashambulio Paris.

04: 27 Rais Francois Hollande amezuru eneo la Bataclan ambako zaidi ya watu 100 wameuawa katika ukumbi wa sanaa. Ameahidi kukabiliana na waliohusika "bila huruma".

Haki miliki ya picha AFP

04:20 Shirika la ndege la Marekani American Airlines laahirisha safari za ndege za kuelekea Paris kutokana na mashambulio mjini humo, shirika la Reuters limeripoti.

"Kwa sasa uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle bado umefunguliwa, hata hivyo, tunasimamisha ndege ambazo hazikuwa zimeondoka jioni hii kuelekea Paris hadi tupate habari zaidi," msemaji wa American Airlines Joshua Freed amenukuliwa na shirika hilo.

Wizara ya mashauri ya kigeni Ufaransa imeambia Reuters kwamba viwanja vya ndege vitabaki kufunguliwa, na safari za ndege na treni zitaendelea.

04:12 Nukuu kutoka kwa taarifa ya Obama: Obama: "Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja. Tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia watu wa Ufaransa na mataifa kote duniani kuhakikisha magaidi hawa wanakabiliwa.”

Haki miliki ya picha AP

04:00 Shirika la habari la AFP limenukuu afisi ya Rais ikisema wanajeshi 1,500 zaidi wametumwa Paris

03:53 Rais wa Marekani Barack Obama ameshutumu shambulio hilo sawa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Obama amezungumzia shambulio hilo kutoka ikulu ya White House

03:47 Tunayoyajua kufikia sasa

 • Watu wengi wameuawa kufuatia mashambulio kadha ya mabomu na bunduki Paris
 • Takriban watu 100 wanaripotiwa kuuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan mjini Paris
 • Wengine wamefariki uwanja wa Stade de France, ambako Ufaransa ilikuwa ikicheza na Ujerumani, na pia katika migahawa kadha
 • Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake
 • Raia mjini Paris wametakiwa kusalia manyumbani. Wanajeshi wametumwa maeneo mbalimbali ya mji kushika doria

03:40 Reuters, wakinukuu afisa mmoja wa baraza la jiji la Paris, wamesema waliofariki kufikia sana Paris ni karibu 140. Kituo cha televisheni cha iTele hata hivyo kimesema waliofariki ni 118.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Watu wengi wamejeruhiwa kwenye mashambulio hayo

03:37 Polisi mjini Paris wawasisitizia raia wasitoke nje. Wasalie manyumbani.

03:26: AFP imenukuuu maafisa wa polisi wakisema watu 100 wamefariki kwenye shambulio lililotekelezwa katika ukumbi wa Bataclan.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Duru zinasema washambuliaji wawili wameuawa

03:20: Rais Hollande amefutilia mbali ziara yake ya Uturuki aliyokuwa ameipanga kuhudhuria mkutano wa G20, kufuatia mashambulio hayo.

03:16 BFMTV, Associated Press na Reuters wote wanaripoti kwamba mateka waliokuwa wamezuiliwa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan wameachiliwa huru.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ambulensi nyingi zilikuwa zimefika Bataclan

03:10 Rais wa Ufaransa Francois Hollande amehutubia taifa moja kwa moja kupitia runinga ya French TV. Ametangaza hali ya hatari.

Haki miliki ya picha AFP

03:00 Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 40 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.

Karibu watu 15 wameuawa karibu na ukumbi wa sanaa wa Bataclan, ambako watu karibu 60 wanashikiliwa mateka.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa uchunguzi wa jinai nje ya uwanja wa Stade de France