Matukio makuu maisha ya Jihadi John

Mwanamgambo wa Islamic State anayejulikana kama Jihadi John jina lake halisi ni Mohammed Emwazi na ni raia wa Uingereza.

 • 1988: Azaliwa Kuwait.
 • 1994: Ahamia Uingereza
 • 2009: Afuzu na shahada ya kwanza katika masuala ya kompyuta chuo kikuu cha Westminster
 • Agosti 2009: Asafiri Tanzania na marafiki zake wawili lakini wanazuiwa kuingia katika uwanja wa Dar es Salaam. Wanapandishwa ndege ya kuelekea Amsterdam, Uholanzi. Huko baada ya kuhojiwa, arejea Dover
 • Sept 2009: Aenda Kuwait kuishi na familia ya babake
 • Julai 2010: Arejea Uingereza kukaa kwa muda tu lakini ananyimwa visa ya kurejea Kuwait.
 • 2012: Apita mtihani wa Celta wa kufundisha lugha ya Kiingereza
 • 2013: Abadilisha jina lake na kuwa Mohammed al-Ayan. Ajaribu kusafiri Kuwait lakini anazuiwa. Atoweka. Wazazi wake waripoti kwa polisi kwamba hajulikani aliko. Polisi waambia familia miezi mine baadaye kwamba alienda Syria.

Video za mauaji alizoonekana

 • Agosti 2014: Video ya kuuawa kwa mwanahabari wa Marekani James Foley
 • 2 Septemba 2014: Video inayoonyesha mwanahabari wa Marekani Steve Sotloff iakikatwa shingo
 • 13 Septemba 2014: Video ambayo inaonyesha mfanyakazi wa misaada wa Uingereza David Haines akikatwa shingo
 • Oktoba 2014: Video ambako mfanyakazi wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning anaonekana akikatwa shingo
 • Novemba 2014: Video ambayo Jihadi John anaonyeshwa akimuua mwanajeshi wa Syria. Kadhalika, inaonyesha mwili wa mfanyakazi wa misaada wa Marekani Abdul-Rahman Kassig, anayejulikana pia kama Peter Kassig
 • 20 Januari 2015: Video ambayo Jihadi John anaonekana akisimama na mateka wawili wa Japan akidai kulipwa kikombozi ili waachiliwe huru
 • 31 Januari 2015: Video inatolewa ikionekana kuonyesha Jihadi John akimkata shingo mateka Mjapani Kenji Goto