Alshabaab lawaua wanajeshi 13 Somalia

Haki miliki ya picha d
Image caption Wapiganaji wa Alshabaab

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab nchini Somali, wameshambulia kambi yenye chuo cha wanajeshi kusini mwa nchi na kuwauwa wanajeshi 13.

Wanajeshi wa Somalia walipambana na washambuliaji hao kwa saa tatu, na wameweza kuilinda kambi,karibu na mji wa Kismayo, wenye bandari.

Wanajeshi 7 walijeruhiwa na wapiganaji 10 waliuwawa.