Tisa wakamatwa shambulio la Lebanon

Image caption Shambulio la Lebanon

Idara za Usalama nchini Lebanon zimefanikiwa kuwakamata watu tisa wanaodhaniwa kuhusika katika shambulio la Lebanon Alhamisi.

Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

Saba kati ya tisa wanaoshikiliwa ni raia wa Syria huku wengione wawili wakiwa raia wa Lebanon.

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo.

Wachunguzi wamebaini kuwa washambuliaji hao waliilenga hospitali inayoendeshwa na taasisi ya wapiganaji wa majeshi ya Kilebanon ya madhehebu ya Shia, Hezbollah.

Hata hivyo shambulio lao halikufanikiwa kutokana na kuimarishwa kwa hali ya usalama hali iliyosababisha kugunduliwa kwa vilipuzi vyao katika mitaa jirani na eneo hilo.