Poland na Slovakia zakataa kupokea wakimbizi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Poland na Slovakia zakataa kupokea wakimbizi kufuatia mauaji ya watu 139 huko Paris

Wakuu nchini Poland na Slovakia wanasema hawataki tena kutekeleza makubaliano ya Ulaya, kuwapokea maelfu ya wakimbizi waliowasili kutoka Afrika na Mashariki ya Kati katika miezi ya karibuni.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Slovenia tayari imeanza kujenga ua ilikuwazuia wakimbizi zaidi

Mataifa hayo yametoa ilani hiyo muda mchache baada ya rais wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker, kushauri kuwa hakuna haja ya kubadilisha sera ya umoja huo kuhusu wahamiaji, baada ya mashambulio ya Paris.

Akizungumza nchini Uturuki, ambako viongozi wa nchi 20 zenye uwezo mkubwa zaidi kiuchumi za G20 wanakutana, Bwana Juncker alisema watu waliohusika na ghasia ni wahalifu, wala siyo wakimbizi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker

Mmoja wa washambuliaji, ametambulika kuwa ni raia wa Syria, ambaye aliingia Umoja wa Ulaya, kupitia Ugiriki, majuma sita yaliyopita kama mhamiaji mkimbizi.