Miili ya Waafrika 15 yapatikana Sinai Misri

Image caption Miili ya Waafrika 15 yapatikana Sinai Misri

Polisi wa Misri wanasema wamegundua miili ya wa-Afrika 15, ambao inaonekana walipigwa risasi na kuuawa, kaskazini mwa rasi wa Sinai.

Wahamiaji wengine wanane walikutikana wahai lakini wamejeruhiwa.

Haijulikani nani aliwashambulia karibu na mji wa Rafah.

Daima kuna mvutano katika eneo hilo, ambako jeshi la Misri linajaribu kupambana na wapiganaji wa Islamic State.