Rais wa Myanmar kupokeza upinzani madaraka

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Myanmar, Thein Sein ameahidi kutoa madarakani

Rais wa Myanmar, Thein Sein,amesema shughuli za kukabidhiana madaraka kwa chama pinzani kilichonyakua ushindi mkubwa katika uchaguzi wa hivi mazuri nchini humo, utatafanyika kwa amani na utulivu.

Ni mara ya kwanza rais huyo kuonekana hadharani tangu chama cha kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi kishinde kwa kishindo Uchaguzi huo wa Jumapili iliyopita.

Uchaguzi huo ambao umetajwa kama uliofanyika kwa uhuru na haki ulikuwa wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 iliyopita .

Rais Sein pia amesema mchakato wa kufanya mabadiliko ya kisiasa pia utakabidhiwa chama kilichoshinda cha NLD.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kiongozi wa Upinzani nchini Myanmar Aung san Suu Kyi

Thein Sein " Maswala yetu ambayo ni wajib wa taifa kutekeleza yatakabidhiwa kwa serikali ijayo kwa mujibu wa utaratibu uliopo''.

''Shughuli yote itafanyika kwa ulaini na utulivu hamna haja ya kuwa na wasiwasi wowote "

Japo chama hicho kimeshinda viti vya kutosha kuwawezesha kuchagua rais pamoja na baraza la mawaziri, katiba ya nchi hiyo haimruhusu bi Suu Kyi kuchaguliwa kama rais kwa sababu bibi huyo mwenye watoto wawili na mumewe si wa kutoka kwa jamii ya wa -myanmar asilia.