FIFA yampiga marufuku miaka 10 afisa wa Nepal

Haki miliki ya picha Ganesh Thapa Facebook
Image caption FIFA yampiga afisa wa Nepal marufuku ya miaka 10

Ganesh Thapa, mmoja wa maafisa wenye ushawishi mkubwa zaidi katika soka ya bara Asia amepigwa marufuku na FIFA ya miaka kumi kwa tuhuma za ufisadi.

Rais huyo wa shirikisho la soka la Nepal mwenye umri wa miaka 55 amepigwa marufuku kushiriki shughuli zote za soka katika kipindi hicho.

Shirikisho la soka duniani FIFA limetoa kauli hiyo baada ya kuibuka madai ya ufisadi.

Ganesh Thapa anashtumiwa kuwa alipokea hongo ili kufanikisha uchaguzi wa wajumbe wa bara Asia katika kamati kuu ya shirikisho la soka duniani FIFA.

Aidha Thapa ambaye ni mbunge nchini Nepal, anachunguzwa na maafisa wa kupambana dhidi ya rushwa kwa tuhuma za kujilimbikizia mamilioni ya dola fedha ambazo zilinuiwa kumarisha soka nchini humo.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Thapa ameiambia BBC kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa FIFA

Ameiambia BBC kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa FIFA

Mwenyekiti wa shirikisho la soka la Lao , Viphet Sihachakr amepigwa marufuku ya miaka 2.

FIFA inadai kuwa Sihachakr "aliitisha kiinua mgongo kutoka kwa afisa mwenza iliapate uungwaji mkono katika uchaguzi wa wanakamati wa shirikisho la kandanda la Asia mwaka wa 2011.