Uingereza kuongeza fedha za kupambana na ugaidi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uingereza kuongeza fedha za kupambana na ugaidi

Waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne amesema kundi la wanamgambo wa Islamic State wanajaribu kuzindua shambulio kubwa la kimtandao wakilenga Uingereza.

Akihutubia shirika la kiintelenjisia la Uingereza GCHQ Osborne amesema kupambana na kundi la IS inamaanisha kukabiliana na tishio dhidi ya kiteknologia za mawasiliano,na silaha nyengine kama bunduki, mabomu na visu.

Osborne amesema Uingereza itaongeza maradufu uwekezaji katika usalama wa kimitandao, ili kukabiliana na hatari ongezeko ya shambulizi la kimitandao kutoka kwa wanamgambo wa jihad wa Islamic State.

Osborne, anasema ili kukabiliana na I-S, inamaanisha ni kudhibiti hatari katika teknolojia ya mtandao kwa pamoja.

Image caption Bwana Osborne ametangaza dola bilioni tatu zitatumika kudhibiti usalama

Bwana Osborne ametangaza dola bilioni tatu zitatumika kudhibiti usalama wa kimitandao katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mapema leo Jumanne, waziri mkuu David Cameron, aliahidi kiwango sawa na hicho ili kuboresha vikosi maalum kama vile kikosi maalum cha makomando SAS ili kukabiliana na ugaidi.