Tunisia yatibua shambulio la kigaidi

Haki miliki ya picha Jeff J Mitchell Getty Images
Image caption Shambulio Tunisia

Mamlaka nchini Tunisia imesema kuwa imewakamata wapiganaji 16 na kutibua shambulio ambalo huenda lingekuwa kubwa kuwahi kutokea mwezi huu.

Maafisa wanasema wale waliokamatwa walikuwa wamefunzwa nchini Libya na Syria na kwamba walikuwa wanapanga kushambulia mahoteli na maeneo ya usalama katika mji wa kitalii wa Sousse.

Eneo hilo lilshambuliwa na wapiganaji hao mapema mwaka huu ambapo takriban watalii 40 waliuawa.