Wapewa talaka kwa kuunga CCM Zanzibar

Haki miliki ya picha Zanzibar Electoral Commission
Image caption Kuhesabiwa kwa kura Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu uliopita

Takriban wanawake 14 kutoka kisiwani Zanzibar nchini Tanzania wanaotuhumiwa kukiunga mkono chama tawala cha mapinduzi CCM katika uchaguzi uliopita kinyume na matakwa ya waume zao wamepewa talaka.

Kulingana na gazeti la Zanzibar daily Newspaper.

Watalakiwa hao wamesema kuwa wanaume zao waliamua kuwapatia talaka nyakati tofauti kutokana na tofauti za kisiasa kwa mujibu wa gazeti hilo.

Limeongezea kwamba wanaharakati kutoka kwa muungano wa mawakili wanawake kisiwani pamoja na mungano wa wanahabari wa kike nchini Tanzania wamesikia kuhusu visa kama hivyo na wameahidi kufuatilia swala hilo.