Facebook yafungua tena kipengele cha usalama

Haki miliki ya picha
Image caption Kipengele cha usalama cha facebook

Mtandao wa facebook umefungua tena kipengele chake cha usalama kufuatia mlipuko m'baya wa bomu lililowauawa takriban watu 32 kaskazini mashariki mwa mji wa Yola nchini Nigeria.

''Tumefungua tena kipengele hicho cha usalama kufuatia mlipuko wa Nigeria,alisema mkurugenzi mkuu wa facebook Mark Zuckerberg.Hasara ya maisha ya binaadamu mahali popote ni janga,na tuko tayari kusaidia ili kuwanusuru watu wengi walio katika janga hilo'',aliongezea.

Mtandao huo wa kijamii ulikosolewa sana kwa upendelo baada ya kufungua kipengele hicho cha usalama kufuatia shambulio la mjini Paris lililowauwa watu 129 siku ya ijumaa,kwa kuwa kipengele hicho hakikufunguliwa wakati wa matukio mengine kama hayo.

Kipengele hicho hufunguliwa ili kuwaonyesha wanaokitumia kwamba wako salama wakati wa matukio kama hayo.