IS wawaua mateka wawili

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mateka waliouawa na IS

Wapiganaji wa kundi la Islamic State limesema kuwa limewaua mateka wengine wawili waliokuwa wanashikiliwa na kundi hilo ambapo kati yao mmoja ni raia wa China na mwingine Norway.

Katika taarifa yao IS wanasema kuwa wamefikia hatua ya kuwaua mateka hao kutokana na serikali zao kushindwa kulipa kiasi cha fedha walichotakiwa kama sehemu ya kuwakomboa mateka hao. Kundi hilo pia limechapisha picha zinazoonyesha miili ya watu wanaonekana kama wameuawa kwa risasi. Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg amesema kutokana na vielelezo inaonyesha kuwa aliyeuawa ni raia wa nchi yake Ole Johan Grimsgaard-Ofstad.Waziri wa mambo ya nje wa China amesema kuwa amepokea kwa mshituko taarifa hizo za mauaji.