Anayedaiwa kufuja fedha za B Haram kukamatwa

Image caption Boko Haram

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameagiza kukamatwa kwa afisa mmoja mkuu serikalini kwa tuhuma za kuiba zaidi ya dola bilioni 2 zilizotengewa vita dhidi ya kundi la Boko Haram.

Kanali Sambo Dasuki ambaye alikuwa mshauri wa kitaifa kuhusu maswala ya usalama kwa aliyekuwa rais Goodluck Jonathan ,ameshtakiwa kwa kutoa kandarasi bandia za kununua helikopta 12,ndege 4 za kijeshi na silaha.

Lakini vifaa hivyo havijawasili na mshauri huyo wa zamani anadaiwa kuiba fedha hizo.Tayari amekana madai hayo.

Msemaji wa rais Buhari ameiambia BBC kwamba ufisadi huo ulisababisha vifo vya maelfu ya raia wa Nigeria.

Wanajeshi wa taifa hilo wamelalamika kwamba licha ya kiasi kikubwa cha fedha kinachotumiwa kununua vifaa vya kijeshi hawana vifaa vya kuweza kukabiliana na kundi la Boko haram.