Mwanamke azuiliwa Costa Rica juu ya hati

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Costa rica

Mamlaka za nchini Costa Rica zinamshikilia mwanamke mmoja mwenye asili ya Ugiriki kwa kosa la kuwa na hati bandia za kusafiria.

Tukio hilo limejiri siku mbili baada ya kukamatwa nchini Honduras kwa wanaume watano wenye asili ya Syria, ambao walikuwa wanajaribu bahati yao kusafiri kuelekea nchini Marekani kwa kutumia pia hati bandia.

Mamlaka za uhamijia nchini humo zimesema kwamba mwanamke huyo aliwasili nchini humo kwa njia ya anga akitokea Peru.

Wakati mwanamke huyo akikamatwa, wanaume hao waliokamatwa kabla yake na mabao bado wanashikiliwa Honduras ,wachunguzi wanadai kwamba wanne kati yao ni wanafunzi na mmoja ni mfanyakazi mwenye utaalamu.

Mamlaka hizo zinaamini kwamba wanaume hao ni wakimbizi waliokimbia Syria,na kwamba hakuna ushahidi wowote kuwa ni wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa kiislam.