Misikiti ya Canada na US yakabiliwa na tishio

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msikiti nchini Australia

Misikiti nchini Marekani na Canada inakabiliwa na ongezeko la uharibifu na vitisho tangu shambulio la Paris.

Vituo vya kiislamu vimekuwa vikipokea ujumbe wa chuki katika simu huku baadhi ya misikiti ikichapishwa michoro ya moto na ujumbe za kulipiza kisasi.

Nchini Canada,mtu mmoja amekamatwa na maafisa wa polisi baada ya kutishia kuwaua waislamu huko Quebec.

Akiwa amejifunika uso wake,aliongezea kuwa atamuua ''mwarabu mmoja kila wiki''.

Ongezeko hilo la matamshi dhidi ya waislamu limetokea baada ya watu 129 kuuawa huku wengine 350 wakijeruhiwa katika mashambulizi ya bunduki na mabomu.

''Hali inaendelea kuwa mbaya'',alisema Ibrahim Hooper wa baraza la uhusiano wa raia wa Marekani na Uislamu{CAIR}.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waandamana kupinga shambulio la msikiti

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema kuwa ''anasumbuliwa'' sana baada na hali hiyo baada ya moto kuwashwa kimakusudi katika msikiti wa muungano wa waislamu wa Kawartha katika mji wa Peterborough,Ontario.

Canada ''itafanya kila juhudi kuwakamata washukiwa'',alisema.