Ripoti: Boko Haram laipiku IS kwa mashambulizi

Haki miliki ya picha Screen Grab
Image caption Kundi la Boko Haram

Ripoti mpya inasema kuwa kundi la Boko Haram limewapiku washirika wao wa Islamic State kama kundi hatari zaidi lenye msimamo mkali duniani.

Ripoti hiyo ya Global Terrorism Index imesema kuwa kuna ongezeko la asilimia 300 ya vifo vinavyohusishwa na mashambulio ya kundi la Boko haram tangu mwaka uliopita.

Utafiti huo uliofanywa na taasisi ya kiuchumi na Amani mjini New York inasema kuwa mashambulio ya kigaidi yameongezeka maradufu katika kipindi hicho ,huku waathiriwa wengi wakitoka mataifa matano-Iraq,Nigeria,Afghanistan,Pakistan na Syria.

Haki miliki ya picha Boko Haram Twitter
Image caption Boko Haram

Ripoti hiyo inasema kuwa kundi la wapiganaji wa Islamic State na washirika wake wanahusishwa na nusu ya visa vya vifo duniani.

Huku mashambulo yakifanyika sana nchini Iraq,ni Nigeria iliokuwa na ongezeko la visa vingi vya kigaidi mwaka 2014.

Boko Haram ambalo linajulikana kama tawi la Islamic state Magharibi mwa Afrika,lilitekeleza mashambulio 20 mabaya zaidi mwaka uliopita.

Haki miliki ya picha Islamic State
Image caption Islamic State

Mashambulio hayo ni pamoja na uvamizi wa mji wa Gamboru Ngala nchini Nigeria.

Zaidi ya watu 300 waliuwawa na wengine wengi wakijeruhiwa huku eneo kubwa la mji huo pia likiharibiwa.

Tukio jingine ni lile la Sudan Kusini,ambapo waasi waliwauwa watu wengi waliokuwa wakichukua hifadhi katika msikiti mmoja katika mji wa Bentiu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa islamic state

Mataifa yenye visa vibaya zaidi vya ugaidi pia yalikuwa na idadi kubwa ya watu waliowachwa bila makao na kuhusisha mashambulio hayo na mgogoro wa wakimbizi.

Ripoti hiyo pia inasema kwamba waendeshaji wa ugaidi katika mataifa yalioyukuwa wanatofautiana na wale kutoka kwa mataifa yanayoendelea.