Martial na Rooney kutocheza wikendi

Image caption Martial na Rooney

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amesema kuwa mshambuliaji Anthony Martial na nahodha Wayne Rooney ni miongoni mwa wachezaji watano ambao hawatashirii katika mechi ya timu hiyo dhidi ya Watford siku ya jumamosi.

Martial mwenye umri wa miaka 19 amejeruhiwa katika mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Uingereza siku ya jumaane huku Rooney akiwa anaugua.

Michael Carrick ,aliyejeruhiwa katika mechi ya kirafiki kati ya Uingereza dhidi ya Uhispania,anajiunga na Marouane Fellaini na Antonio Valencia katika meza ya matibabu.

Van Gaal aidha amesema kuwa mshambuliaji James Wilson hayuko tayari kucheza dakika 90 kutokana na jereha.

Martial pia alicheza katika mechi kati ya Ufaransa na Ujerumani katika uwanja wa Stade de France ijumaa iliopita,mechi iliolengwa ikwa miongoni mwa mashambulio ya Paris.

Watu 3 walifariki nje ya uwanja huo,huku wengine 129 wakiuawa katika mashambulio tofauti mjini humo.

Lakini Van Gaal amesema kuwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Morgan Schneiderlin na kiungo wa kati wa Ujerumani Bastain Shweinsteiger,ambao walicheza katika mechi hiyo watashiriki .