Kiongozi wa shambulizi la Paris 'alikuwa mlevi'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Abaaoud

Mshukiwa aliyeongoza mashambulio ya kigaidi mjini Paris Abdelhamid Abaaoud,alionekana akinywa pombe na kuvuta bangi na watu wengine nje ya nyumba yake baada ya mauaji hayo.

Walonekana wakivuta bangi na kunywa pombe, ''huonekana katika barabara kila mara..sasa nawajua,sasa nawajua'', mmoja ya mashahidi alikiambo chombo cha habari cha Sky News.

Shahidi mwengine aliliambia gazeti la Daily Mail nchini Uingereza :''Alikuwa barabarani na chupa ya pombe aina ya whiskey na aliniomba ninywe''.

''Niligundua kwamba alikuwa mtu wa iana gani baadaye''.

Abaaoud aliuawa wakati wa uvamizi wa polisi katika nyumba yake iliopo St. Denis siku ya Jumatano.