Mwili wa mshukiwa wa 3 wa ugaidi wapatikana

Haki miliki ya picha
Image caption Nyumba iliokuwa ikiishi washukiwa wa shambulio la ugaidi mjini Paris

Mwili wa 3 umepatikana katika nyumba ya Saint-Denis iliovamiwa na maafisa wa polisi kuhusiana na shambulizi la Paris,kulingana na kiongozi wa mashtaka nchini humo.

Vilevile amethibitisha kuwa mwanamke mmoja ni miongoni mwa watu watatu waliouawa,huku pasipoti ilio na jina la Hasna Aitboulahcen ilipatikana katika handi begi yake katika eneo hilo.

Haki miliki ya picha
Image caption Usalama waimarishwa Paris

Mwili mmoja umetambulika kuwa wa kiongozi wa shambulio hilo Abaaoud Abdelhamid.