China:Marekani inachochea mataifa ya Asia

Haki miliki ya picha z
Image caption China imetetea hatua yake ya kujenga viwanja vya ndege katika bahari ya kusini mwa China

Uchina imeishutumu Marekani kuwa inafanya uchochezi wa kisiasa, kwa kupiga doria katika eneo linalozozaniwa la bahari ya kusini ya Uchina.

Naibu waziri wa mashauri ya nchi za nje, Liu Zhenmin, alisema hayo katika mkutano wa Jumuia ya nchi za Asia Mashariki, ASEAN, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani imetuma manowari na ndege katika eneo hilo katika majuma ya karibuni, ikisema kuwa inataka kusisitiza uhuru wa safari za meli

Swala kubwa katika mkutano huo ni madai ya Uchina ya ardhi katika bahari ya kusini ya Uchina, ardhi ambayo inadaiwa na nchi za jirani pia.

Marekani imetuma manowari na ndege katika eneo hilo katika majuma ya karibuni, ikisema kuwa inataka kusisitiza uhuru wa safari za meli katika bahari hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchina imekuwa ikijenga visiwa kusisitiza madai yake.

Uchina imekuwa ikijenga visiwa kusisitiza madai yake.