Real Madrid 0-4 Barcelona El Clasico

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Suarez alifunga mabao mawili

Baada ya kuambulia kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Barcelona, vigogo wa soka ya Uhispania Real Madrid wanahitaji kuuguza majeraha yao kwa haraka.

Kocha wa Madrid,Rafael Benitez anashauri vijana wake wasiomboleze sana kufuatoa kichapo hicho cha El Clasico.

''Tunahitaji kujifurukuta na kuhakikisha mechi yetu ya baadaye itakuwa ya ufanisi''

Benitez ambaye alikuwa anashiriki mechi yake ya kwanza ya El Clasico anasema kuwa, aliwashirikisha wachezaji wake nyota,James Rodriguez, Gareth Bale na Karim Benzema.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Real Madrid 0-4 Barcelona El Clasico

''Bila shaka tulifanya makosa makubwa ambayo tuliadhibiwa vilivyo'' alisema Benitez.

Mabao mawili ya Luis Suarez katika uwanja wa Santiago Bernabeu lingine la Neymar na kiziba mkonga kutoka kwa Andres Iniesta yaliisaidia the Catalans kujikita kileleni mwa jedwali la La Liga wakiwa na pengo la alama 6 zaidi ya wapinzani wao wa jadi.

Kinyume na matarajio ya wengi, Lionel Messi alianza mechi hii akiwa mchezaji wa akiba lakini hilo halikuizuia Barcelona kutamba mbele ya mahasimu wao.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kichapo hicho kilikuwa cha kwanza kwa Real Madrid katika mechi 23 za ligi hiyo ya Uhispania uwanjani Santiago Bernabeu.

Kichapo hicho kilikuwa cha kwanza kwa Real Madrid katika mechi 23 za ligi hiyo ya Uhispania uwanjani Santiago Bernabeu.

Hata hivyo wadadisi wanahoji tayari uwezo wa vijana hao wa Benitez kushindana dhidi ya Barca kwa taji la msimu huu.

Real wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na alama 24 huku Barcelona ikiongoza kwa alama 30 baada ya mechi ya 12.

Real sasa wanakabiliwa na upinzani mkali katika mechi yao ijayo dhidi ya Shakhtar Donetsk katika ligi ya mabingwa.

Aidha Real wanaratibiwa kuchuana dhidi ya Eibar katika La Liga kabla ya kupimana nguvu dhidi ya Cadiz katika mechi ya kombe la Copa del Rey.