Obama aapa kuiangamiza IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marekani na washirika wake wataiangamiza Islamic State.

Marekani na washirika wake wataiangamiza Islamic State.

Rais Barack Obama amesema kuwa Marekani na washirika wake hawatalegeza vita vyao dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu wa Islamic State.

Akiongea kwenye mkutano wa nchi za kusini mashariki mwa Asia ASEA,mjini Kuala Lumpur bwana Obama amesema kwa Marekani itaendelea kuongoza vita dhidi ya wanamgambo hao na kuwapokonya ardhi walioitwaa kabla ya kuwaandama viongozi wake na kuiangamiza kabisa.

Obama amesema kuwa mashambulizi ya Paris hayatakubaliwa na Islamic State wataangamizwa.

Obama aliitaka Urusi kuelekeza jitihada zake katika kuiangamiza Islamic State.

''Hatutakubali watu tuliowashinda katika viwanja vya kivita kurudi nyuma yetu na kuwaua raia ambao hawana hatia katika mikahawa majumba ya sinema na watoto wetu'' alisema Obama.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Obama aliitaka Urusi kuelekeza jitihada zake katika kuiangamiza Islamic State.

''Hawa ni watu waoga wauaji ambao hata hawana utu''

''Angalia walichokifanya huko Paris, kwa hakika hatutawaruhusu waendelea kufikiria na kuota ndoto ya kuwa hiyo ni kawaida''

'sharti sote tufanye jambo la kuwatahadharisha Islamic State iliwasidhanie kuwa tumeogopa'' alisema Obama.