Meya ashinda Argentina

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Meya akishangilia ushindi

Meya wa mji wa Buenos Aires Mauricio Macri ameshinda uchaguzi wa urais nchini Argentina katika duru ya pili ya uchaguzi huo.

Mshindani wake makamu wa rais wa zamani Daniel Scioli amekubali kushindwa. Akihutubia wafuasi wake bwana Macri aliwashukuru wapiga kura na kuahidi kafunya mabadiliko. Amesema kuwa nchi hiyo imeingia kipindi kipya.

Kushindwa kwa Scioli kunamaliza kipindi cha miaka 12 cha serikali ya rais wa zamani Cristina Fernandez de Kirchner na mumewe hayati Nestor Kirchner.