Huduma ya kulipa wanaotembea yazinduliwa Afrika

Haki miliki ya picha
Image caption Programu ya Bitwalking itakayowalipa watu kutembea yazinduliwa Kenya na Malawi

Hivi karibuni utakuwa ukilipwa kutokana na umbali unaotembea kwa mwezi mmoja baada ya hatua unazofanya kila siku kujumlishwa.

Sarafu za kidigitali ama 'Bitwalking dollars' ( BW$) zitakuwa zikitolewa baada ya programu ya simu kuhesabu na kudhibitisha idadi ya hatua ambazo umechukua kwa umbali fulani.

Hatua 10,000 ambazo ni takriban maili tano zitakupa kipato cha 1BW$, hela ambazo utatumia kununua bidhaa mitandaoni ama kuzibadilisha na kuwa pesa taslimu.

Waanzilishi wa mradi huo Nissan Bahar na Franky Imbesi wamefaulu kupata ufadhili wa dola milioni kumi kutoka kwa wawekezaji wa Japan zitakazotumika kuzindua sarafu hiyo ya dijitali na pia kutengeneza benki ya kuthibitisha hatua na uhamisho wowote wa fedha.

Kampuni maarufu ya kielektroniki ya Japan imeanza kutengeneza kifaa cha kufunga mkononi kitakachotumika kuhesabu kwa urahisi kiasi cha fedha ambazo mtu amefaulu kupata.

Waanzilishi wa mradi huo wanapanga kushirikiana na kampuni za kutengeneza bidhaa za michezo, kampuni za kutoa huduma za afya, kampuni za bima ya afya na kampuni nyinginezo.

Haki miliki ya picha
Image caption Mbali na Kenya na Malawi programu hiyo ya Bitwalking itazinduliwa pia Japan na Uingereza

Katika mataifa yaliyostawi, mtu wa kawaida anakadiriwa kuzoa kipato cha 15BW$ kila mwezi.

Katika mataifa yanayoendelea ambapo inawabidi watu kutembea kwa umbali mrefu kwenda kazini, shuleni na katika shughuli za kila siku, basi mradi huu wa kupata hela kwa matembezi utayafaa maisha ya wengi.

Kipato mara mbili.

Salim Adam hutembea umbali wa kilomita kumi kila siku kwenda kazini katika eneo la Mthuntama Kaskazini mwa Malawi.

Hesabu zinaonyesha kuwa atapata dola 26 za kutembea (BW$) iwapo ataweka programu hiyo kwenye simu yake.

Image caption Mwaka waliopita walizindua kifaa kinachotumika kama kompyuta mjini Nairobi Kenya

Kwa sasa mshahara wake ni dola 26.

Waanzilishi wa mradi huu wanajua manufaa yake hasa katika mataifa yanayoendelea na ndiposa wakauanzisha.

Malawi ni mojawapo ya mataifa ya AfriKa yatakayoshirikishwa katika uzinduzi wa mradi huo, taifa ambalo mshahara wa kila siku kwa watu wa maeneo ya mashinani ni dola 1.5.

Karen Chinkwita ni mshauri wa kibiashara katika eneo la Lilongwe nchini Malawi anasema

"kuna uwezekano wa majaribio kuwa watu watembea badala ya kufanya kazi"