Blatter asema alinusurika kifo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Blatter asema alinusurika kifo

Rais aliyepigwa marufuku wa shirikisho la soka duniani,FIFA,Sepp Blatter amesema alinusurika kifo kufuatia matatizo ya kiafya yaliyomkumba majuzi.

Suspended Fifa president Sepp Blatter has said he feared he was dying during a recent health scare.

Blatter, 79, ambaye anatumikia marufuku ya siku 90 kutoka kwenye maswala yeyote ya kandanda alilazwa kwa siku 6 hospitalini akiwa amezongwa na msukumo wa maisha.

''nilikuwa katikati ya malaika walokuwa wakiimba kwa furaha na sheitan aliyekuwa akiwasha moto lakini malaika ndio walioimba'' alisema Blatter.

'Nilikaribia kufa.'

'Wakati mmoja ulifika ambao mwili ulikubali kushindwa'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Blatter, na Platini wanatumikia marufuku ya siku 90 kufuatia malipo yaliyoihujumu FIFA

Blatter, ambaye ameiongoza FIFA kwa zaidi ya miaka 18 alipigwa marufuku ya kushiriki maswala yeyote ya kandanda kufuatia kupatikana kwake na hatia ya kumlipa rais wa shirikisho la soka la UEFA Michel Platini fedha kinyume cha maadili ya FIFA.

Kamati ya maadili na nidhamu ya FIFA inachunguza malipo ya pauni milioni 1.35 kwa Platini.

Blatter na Platini wanakanusha kukiuka sheria na madai yeyote dhidi yao.