Aliyeokolewa baada ya siku 41 mgodini afariki

Migodi
Image caption Wachimbaji migodi wenzake wanne wanaendelea kupata nafuu

Mmoja wa wachimbaji migodi waliookolewa baada ya kufukiwa na vifusi ameaga dunia.

Madakatari waliomuhudumia wanasema kuwa, Onyiwa Morris, 55, alikuwa na matatizo makubwa ya utumbo kutokana na ukosefu wa chakula kwa muda mrefu.

Manusura wengine wanne, bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali kuu ya mkoa wa Kahama magharibi mwa Tanzania ambapo daktari wanaowahududumia wanasema wanaendelea kupata nafuu.

Watanzania wengi wameguswa na yalowafika wachimbaji hawa na wamekuwa wakifika hospitalini kuwaona wagonjwa na kuwaletea zawadi ndogo ndogo kama maji na matunda.

Wagonjwa hao wanasema watahitaji msaada watakapo toka hospitalini maana ndugu ambao walikuwa wamepoteza matumaini ya wao kuwa hao walishagawa mali zao.