Putin azuru Iran kujadili hatma ya Syria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Urusi na Iran ndio mataifa yanayounga mkono utawala wa rais wa Syria,Bashar al-Assad.

Rais wa Urusi Vladimir Putin anazuru Tehran kwa mazungumzo na kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei kuhusiana na mapigano yanayoendelea nchini Syria.

Urusi na Iran ndio mataifa yanayounga mkono utawala wa rais wa Syria,Bashar al-Assad.

Urusi imekuwa ikiendeleza vita vya mashambulizi ya angani dhidi ya Islamic State na hata dhidi ya vikosi vya wapinzani wa Bashar al Assad.

Image caption Urusi imekuwa ikiishambulia IS kwa makombora ya mbali

Vikosi vya Iran kwa upande wao vimekuwa vikisaidia wanajeshi wa Syria wa ardhini.

Wakati huohuo safari za ndege za raia wa eneo la Mashariki ya kati zimevurugwa kutokana na mashambulizi ya angani yanayofanywa na Urusi dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Syria.

Viwanja vya ndege Kaskazini mwa Iraq vimefungwa kwa siku mbili na safari za ndege kutoka na kuingia kwenye mji mkuu wa Lebanon, Beirut zikihamishwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Putin azuru Iran kujadili hatma ya Syria

Utawala wa maeneo ya kikurdi nchini Iraq umetoa malamishi yake kwa Urusi baada ya makombora ya majeshi yake kupitia kwenye anga yake kuendesha mashambulizi hayo.

Kwengineko serikali ya Syria yasema imefaulu kuwazidi nguvu wapiganaji wa IS baada ya makabiliano makali huko Magharibi mwa nchi , na kutwaa miji ya Mheen na Hawwarin .

Miji hiyo miwili iko katika eneo la njia kuu inayounganisha mji mkuu wa nchi hiyo , Damascus na miji mingine ya Kaskazini mwa nchi hiyo.