Waliotoa siri za afisi ya Papa washtakiwa

Image caption Waandishi walioshtakiwa

Watu 5 wamefunguliwa mashtaka katika makao makuu ya kanisa katoliki Vatican,kwa tuhuma za kutoa na kuchapisha nakala za siri zinazoonyesha usimamizi mbaya katika afisi hiyo takatifu.

Waandishi wawili waliopata nakala hizo katika vitabu viwili watakabiliwa na jopo wakiwemo wanachama wawili wa tume ya Papa pamoja na naibu mmoja.

Iwapo watapatikana na hatia huenda wakahudumia kifungo cha miaka minane jela.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Papa Francis

Vyombo vya habari vimeshtumu kesi hiyo.Mmoja wa waandishi aliyefunguliwa mashtaka aliitaja hatua hiyo kama uvamizi wa uhuru wa vyombo vya habari.

Waandishi hao Emiliano Fittipaldi na Gianluigi Nuzzi ,waliandika kuhusu usimamizi m'baya wa fedha za hisani katika vitabu vyao vya Merchants in The Temple na Avarice.

Madai hayo yanaorodhesha uimarishaji wa makao ya makadinali na mengine.

Watatu hao wanaodaiwa kutoa siri za nakala hizo ni raia wa Uhispania padri Angelo Lucio Vallejo Balda,katibu wake na afisa mmoja wa mahusiano ya uma anayekaa katika tume inayomshauri papa huyo kuhusu maswala ya mabadiliko ya kiuchumi .