MOJA KWA MOJA: Uturuki 'yadungua ndege ya Urusi'

Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi

18:01 Waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amefutilia mbali mipango yake ya kuzuru Uturuki Jumatano, mashirika mbalimbali yaripoti. Uturuki imeendelea kusisitiza ndege ya Urusi iliyodunguliwa ilikuwa imeingia anga ya Uturuki, Urusi nayo ikisisitiza ndege hiyo haikuvuka mpaka kutoka Syria.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Bw Lavrov alipangiwa kuzuru Uturuki Jumatano

17:26 Maandamano pia yameshuhudiwa nje ya ubalozi wa Uturuki mjini Moscow

Haki miliki ya picha AP

17:24 Maandamano yashuhudiwa nje ya ubalozi wa Urusi mjini Istanbul

Haki miliki ya picha AFP

17:22 Habari zinasema kuna helikopta ya Urusi ambayo imelazimishwa kutua ghafla baada ya ksuahmbuliwa ikiwa eneo linalodhibitiwa na waasi Syria. Shirika la Syrian Observatory for Human Rights linasema helikopta hiyo imefanikiwa kufika maeneo yanayodhibitiwa na serikali jimbo la Latakia kaskazini mashariki mwa Syria.

17:21 Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu atetea kudunguliwa kwa ndege ya kivita ya Urusi, akisema ni wajibu wa kitaifa kulinda taifa dhidi ya yeyote anayeingilia ardhi na anga ya Uturuki.

Haki miliki ya picha AP

17:20 Shirika la habari la Reuters linasema wizara ya mashauri ya kigeni ya Uturuki imewaita mabalozi wa Marekani, Urusi, Ufaransa, Uchina na Uingereza kuwapasha kuhusu kuangushwa kwa ndege ya Urusi.

17:16 Putin amehitimisha hotuba yake kwa kudokeza kwamba Uturuki inataka Nato "itumikie" Islamic State. Awali alikuwa ameeleza Uturuki kama "washirika wa magaidi".

17:15 Bw Putin: "Tutatathmini kila kitu kwa kina na matukio haya ya leo yataathiri makubwa uhusiano kati ya Urusi na Uturuki."

Haki miliki ya picha Reuters

15:57 Rais wa Urusi Vladimir Putin asema ndege ya kivita ya Urusi mpaka wa Uturuki na Syria imedunguliwa na "washirika wa magaidi." Amekuwa akiongea katika runinga ya serikali ya Urusi ya Rossiya 24.

15:54 Uturuki yadai ramani ya safari za ndege inadhihirisha ndege ya kivita ya Urusi iliingia anga ya Uturuki.

Haki miliki ya picha

15:07 Kundi moja la waasi Syria limepakia mtandaoni video inayoonyesha mmoja wa marubani wa ndege ya Urusi iliyoangushwa Syria akionekana kuwa bila fahamu, akiwa labda ameumia vibaya au kufariki.

15:05 Shirika la habari la AFP laripoti kuwa Nato imeitisha "mkutano maalum" baada ya kuangushwa kwa ndege ya Urusi.

Mkutano huo umeitisha kufuatia ombi kutoka kwa Uturuki, lengo likiwa kufahamisha wanachama wa Nato kuhusu kuangushwa kwa ndege ya Urusi.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanachama wa Nato kuangusha ndege ya Urusi au uliokuwa Muungano wa Usovieti tangu miaka ya 1950, kwa mujibu wa shiriika la habari la Reuters.

15:00 Msemaji wa Wizara ya Kigeni ya Uingereza ametaja kisa cha kuangushwa kwa ndege ya Urusi kuwa “kibaya sana”. Amesema: “Tunatafuta maelezo zaidi. Ni wazi kwamba kisa hiki ni kibaya sana na haitakuwa busara kuzungumzia hadi tuwe na taarifa sahihi.”

14:44 Bei ya mafuta yaanza kupanda kufuatia habari kwamba ndege ya kivita ya Urusi imedunguliwa karibu na mpaka wa Syria na Uturuki. Kudorora kwa dola kumewapa wawekezaji kichocheo cha kununua mafuta zaidi.

"Kuanguka kwa ndege ya kivita Syria ni ukumbusho kwamba bado kuna hatari kubwa Mashariki ya Kati," amesema mtathmini mkuu wa bidhaa katika benki ya SEB anayeishi Norway Bjarne Schieldrop, akizungumza na Reuters.

14:39 Msemaji wa Rais Vladimir Putin, Bw Dmitry Peskov, ametaja kudunguliwa kwa ndege ya Urusi aina ya Su-24 kuwa "kisa kibaya sana", lakini ni mapema mno kusema mengi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Picha mseto zikionyesha kuanguka kwa ndege ya Urusi

14:35 Afisa mmoja wa habari wa Nato amesema shirika hilo "limewasiliana na maafisa wa Uturuki" lakini kwa sasa hakutatolewa taarifa zozote zaidi.

14:30 Wizara ya ulinzi ya Urusi imethibitisha ndege iliyoangushwa ilikuwa muundo wa Su-24.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za Su-24 zimekuwa zikitumiwa na Urusi dhidi ya waasi wanaompinga Rais Bashar al-Assad

14:28: Wanaharakati nchini Syria wamenukuliwa wakisema mmoja wa marubani wa ndege hiyo ya Urusi amekamatwa. Anadaiwa kuzuiliwa katika eneo lenye milima la Utayrah jimbo la Turkmen Mount, kwa mujibu wa Al-Jazeera Arabic TV.

14:20 Ndege za kijeshi za Uturuki zimeripotiwa kudungua ndege ya kijeshi ya Urusi karibu na mpaka wake na Syria.

Haki miliki ya picha ANAD OLU
Image caption Kituo cha Anad Olu kimetoa picha zinazoonyesha ndege hiyo ikianguka

Hujambo! Karibu kwa habari za moja kwa moja kuhusu ripoti za kuangushwa kwa ndege ya Urusi eneo la Syria.