Ufaransa yachunguza mkanda wa kujilipua

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Charles de Gaulle

Polisi wa Ufaransa wanatathmini kile kinachoaminika kuwa ni mkanda wa kujitoa muhanga, uliopatikana kusini mwa mji wa Paris

Watu wanaokusanya taka ndio waliokiona kitu hicho katika pipa la taka huko Montrouge.

Vyanzo vya polisi vinasema, kitu hicho kinafanana na mikanda iliyotumika katika mashambulio ya mjini Paris, ambayo ina sehemu ya mbele na ya nyuma ya kuwekea chaji.

Pia inachunguzwa ili kubaini iwapo mkanda huo ulivaliwa na mshukiwa mkuu Salah Abdeslam.

Wakati huo huo, kwa mara ya kwanza Ufaransa, imepeleka vikosi vyake kupambana na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu IS kupitia meli yake ya kubeba ndege za kijeshi ya Charles de Gaulle.