Yahoo yafungia matangazo ya kibiashara

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yahoo yafungia matangazo ya kibiashara

Baadhi ya watumiaji wa barua pepe wa Yahoo nchini Marekani wameripoti kuwa kampuni hiyo ya Yahoo imekuwa ikiwatumia ujumbe unaowataka wadhoofishe programu inayozuia matangazo ya kibishara ndipo waweze kupata ujumbe wa barua pepe.

Yahoo ilisema ilikuwa inafanya majaribio ya bidhaa mpya nchini Marekani.

Watumiaji wa programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara walisema tayari wamefaulu kukabiliana na kizuizi hicho.

Programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara imekumbwa na utata na kampuni za kiteknologia zimekuwa zikielezea maoni yao kwa njia tofauti.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara imekumbwa na utata na kampuni za kiteknologia

Mnamo mwezi Septemba, kampuni ya Apple iliboresha mfumo wake wa simu za mkononi ili kuruhusu watumiaji wa programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara kuwa na uwezo wa kuutembelea.

Wakati huo huo Google inasema imeanzisha mpango wa malipo kwenye mtandao wake wa YouTube, ambao unawawezesha watazamaji kutoa matangazo yao ya kibiashara kutoka kwenye video kwa malipo ya kila mwezi.

Wakereketwa wa programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara wanasema kudhoofisha matangazo hayo huenda kukarefusha huduma ya betri ya simu aina ya smartphone na kupunguza matumizi ya deta kwenye simu za mkononi.