2015 inaviwango vya juu zaidi vya joto duniani

Haki miliki ya picha WMO
Image caption 2015 inaviwango vya juu zaidi vya joto duniani

2015 ndio mwaka uliorekodi viwango vya juu zaidi vya joto duniani.

Takwimu hiyo ni kwa mujibu wa kitengo cha umoja wa mataifa kinachohusika na utabiri wa hali ya hewa duniani.

Kinachosababisha hali hiyo ni kuzidi kutolewa kwa viwango vya hewa chafu duniani inayosababisha mabadiliko yasiyo na tija.

Moja ya athari zake ni hali ya El Nino ya mvua nyingi kupita kiasi inayosabisha mafuriko au El nina yaani jua na ukame mkali.

Hali hiyo ya joto zaidi imeshuhudiwa hasa miaka ya 2011 na 2015 hivyo kutarajiwa kupanda kwa nyuzi joto moja zaidi kuliko hali ilivyokuwa kabla ya maendeleo yanayotokana na viwanda yaliyokuja na uzalishaji mwingi wa mali lakini pia ukazalisha hewa chafu na mkaa kwa mwingi duniani.

Image caption Moja ya athari zake ni hali ya El Nino ya mvua nyingi kupita kiasi inayosabisha mafuriko au El nina yaani jua na ukame mkali.

Mkutano wa wiki ijayo wa mazingira huko Ufaransa unatarajiwa kulizungumzia hilo kwa kina kutafuta suluhu la pamoja la kukabiliana na tatizo hilo.

Mpango wa biashara wa hali ya anga ya Afrika utawasilishwa katika kongamano la kimataifa litakaloandaliwa mjini Paris mwezi ujao.

Benki la dunia linasema kuwa mikakati hiyo itajumuisha uwezo wa watu wa kuhimili halijoto, kuongeza nishati endelevu barani na kuimarisha njia za utoaji onyo mapema.

Aidha ripoti hiyo inasema kuwa mabadiliko ya hewa huenda ikawa na athari zaidi Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na kusababisha ukame, kuongeza bei ya bidhaa na kudhuru ukuaji wa watoto.

Mshauri mmoja mkuu wa maeneo ya Afrika Jamal Saghir amesema mpango huo unamatumaini.

''Mpango huu unastahili kubadilisha tunavyofanya biashara.

Kufikia sasa, uwekezaji wa dola bilioni tatu umefanyika kuimarisha uzoefu wa mabadiliko ya hali ya anga Afrika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mpango wa biashara wa hali ya anga ya Afrika utawasilishwa katika kongamano la kimataifa litakaloandaliwa mjini Paris mwezi ujao.

Tunaamini tunafaa kwenda kwa mpangoi wa kuwekeza dola bilioni 16 kwa miaka chache ijayo ili kuweza kusuluhisha hili suala kwa umakini.

Naibu Rais wa kanda ya Afrika, Makhtar Diop amesema mpango wa benki ya dunia ni kujaribu kufanikisha mambo matatu Afrika.

''Tunajaribu Kuimarisha ustahimili, kuzidisha ustahimili, na kuwezesha ustahimili. Na kwa hivyo tunamaanisha itakuwa ni fursa ya kusonga hadi njia ya ukuaji iliyoambwa kwa ukulima bora, juu ya ustahimili bora, juu ya usimamizi wa misitu, juu ya usimaizi wa pwani na kusaidia uchumi wa bahari.est year