Kilo 10 ya vilipuzi zilitumika Tunisia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ukanda wenye kilo kumi ya vilipuzi ndio uliotumika katika shambulizi dhidi ya walinzi wa rais nchini Tunisia.

Ukanda wenye kilo kumi ya vilipuzi ndio uliotumika katika shambulizi dhidi ya walinzi wa rais nchini Tunisia.

Haya yamebainika kufuatia uchunguzi wa awali wa shambulizi la bomu katikati ya mji mkuu wa Tunisia,shambulizi lililosababisha vifo vya walinzi 12 wa rais.

Zaidi ya watu wengine 20 walijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo la jioni.

Siku 30 za hali ya hatari imetangazwa nchini humo.

Vilevile amri ya kutotoka nje imetangazwa na rais wa Tunisia.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Siku 30 za hali ya hatari imetangazwa nchini humo.

Maafisa wa usalama nchini Tunisia wanasema kuwa wamegundua kuwa ukanda wenye kilo kumi ya vilipuzi ndio uliotumika katika shambulizi dhidi ya walinzi wa rais.

Taarifa kutoka kwa wizara ya ulinzi wa ndani ume inasema kuwa dalili zote zinaonesha kuwa mlipuaji wa kujitolea muhanga anashukiwa kuwa mmoja wa watu 13 waliokufa katika shambulizi hilo.

Kuna mwili mmoja ambao haujatambulika na wanaendelea kufanya uchunguzi wa chembechembe za DNA ilikubaini ni mwili wa nani.

Watu wengine 12 wamekwisha tambulika kuwa ni maafisa wa kikosi cha kumlinda rais.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulizi hili ni la tatu katika taifa hilo katika kipindi cha miezi 11 iliyopita.

Marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi asubuhi iliyowekwa hapo jana sasa imeongezwa muda.

Shambulizi hili ni la tatu katika taifa hilo katika kipindi cha miezi 11 iliyopita.

Katika shambulizi la mwezi Machi mwaka huu na baadaye mwezi Juni wapiganaji waliwalenga watalii katika mji muu wa Tunis na kisha mji wa pwani ya Sousse.

Hakuna kundi lililodai kutekeleza shambulizi hilo japo mashambulizi ya awali yalidaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Islamic State.