Cameron aomba idhini kukabili IS Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri David Cameron ameihutubia bunge akitaka liidhinishe mashambulizi dhidi ya IS

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amewasilisha hoja zake leo akisisitiza umuhimu kuhusu ni kwa nini Uingereza inapaswa kujiunga na muungano wa mataifa yanayofanya mashambulio ya angani dhidi ya Islamic State nchini Syria.

Akihutubia bunge la nchi hiyo amesema haieleweki kwamba Uingereza ingali inasitasita na kutarajia mataifa mengine yabebe mzigo wa kupigana na Islamic State pekee yao ilhali tishio la ugaidi unakabili ulimwengu mzima,Uingereza ikiwemo.

Bw. Cameron ameuliza hata baada ya mashambulio ya Ufaransa ikiwa Uingereza haitachukua hatua yoyote washirika wetu wataiuliza kama sasa sio wakati mwafaka basi ni lini ?

Hata hivyo baadhi ya wapinzani wamehoji ikiwa mashambulio kama hayo yatapunguza au kuongeza vitisho vya Uingereza kulengwa na kundi hilo.

Image caption Bw. Cameron ameuliza hata baada ya mashambulio ya Ufaransa ikiwa Uingereza haitachukua hatua yoyote washirika wetu wataiuliza kama sasa sio wakati mwafaka basi ni lini ?

Kiongozi wa chama cha leba , Jeremy Corbyn,ameuliza msururu ya maswali kuhusu mpango huo

"Hamna shaka kwamba IS ni tisho hata kwetu ssi Uingereza lakini swali ni je tukielekeza mashambulio yetu Syria hilo ndilo litapunguza au kuongeza tisho la Uingereza kushambuliwa.''

'' je hiyo ndio njia mwafaka ya kukabiliana na Islamic State au itasambaza itikadi kali ya ISIL huko mashariki ya kati?."

Mapema mwezi huu kamati inayohusika na masuala ya kimataifa nchini Uingereza ilisema kuwa hatua za kijeshi za Uingereza nchini Syria haziwezi kufanyika bila ya kuwepo mikakati mizuri ya kulishinda kundi la .