Mmoja kati ya watoto 3 anaolewa mapema Afrika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mmoja kati ya watoto watatu barani Afrika wanaolewa kabla hawajatimia umri wa miaka 18.

Mmoja kati ya watoto watatu barani Afrika wanaolewa kabla hawajatimia umri wa miaka 18.

Shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataafa UNICEF limesema huku katika siku ya ufunguzi wa mkutano wa muungano wa Afrika mjini Zambia.

Idadi hiyo imepungua kwa asiliami 10 ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka 25 iliyopita lakini UNICEF inasema kuwa hakuna hatua zilizopigwa kwenye familia maskini barani Afrika.

Mkutano huo wa AU wa siku mbili ambao una lengo la kutafuta njia za kumaliza ndoa za mapema kwa watoto wa kike barani humo.

Kwa mujibu wa UNICEF familia nyingi zinapendelea wasichana wao waolewe pindi wanapobaleghe badala ya kuendelea na masomo yao.

Idadi hiyo inatarajia kuongezeka ifikapo mwaka 2050.

Mamia ya wasichana wa kike waliokuwa na ndoto za kuenda shule wamejikuta wakilazimika kuwa mama, baada ya kulazimisha kuolewa mapema.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption AU inapendekeza umri wa mapema ambao mwanamke anaruhusiwa kuolewa uwe ni miaka 18.

Nyingi ya ndoa hizo za mapema hufanyika vijijini, ambako utamaduni bado unanguvu.

Umoja wa Afrika na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yameunganisha nguvu kushawishi serikali mbalimbali kufanya ndoa za utotoni kama jambo lisilo halali kisheria, kutokana na kukinza haki ya mtoto kupata elimu na pia kumuathiri afya yake.

Muungano wa mataifa ya Afrika unapendekeza umri wa mapema ambao mwanamke anaruhusiwa kuolewa uwe ni miaka 18.

Muungano huo wa AU unapania kutangaza kuwa haki za watoto ni haki za kibinadamu na kuwa kuwaoza wasichana mapema ni kuhujumu haki za watoto.

Mkutano huo huko Zambia unawaleta pamoja wake wa marais wawakilishi wa mataifa wanachama.