Akatazwa kuvaa hijab kazini Ufaransa

Image caption Wanawake waliovalia Hijab Tajikistan

Mahakama ya Ulaya ya haki za kibinaadamu imekataa hoja ya mfanyikazi mmoja wa kiislamu aliyetaka kuvaa hijab kazini.

Christine Ebrahimian alipoteza kazi yake katika hospitali moja ya Paris baada ya kusisitiza kutaka kuvaa hijab.

Hospitali hiyo ilisema kuwa imepokea malalamishi kuhusu yeye kutoka kwa wagonjwa.

Sheria ya Ufaransa inakataza wazi maonyesho ya uhusiano wowote wa kidini na wafanyakazi wa umma .

Mahakama hiyo imesema kuwa haiwezi kutoa hukumu kuhusu sheria za wafanyikazi na kukataa rufaa yake.