Watoto wapewa jina la Papa Kenya

Akina mama kadhaa katika mji wa Kakamega uliopo magharibi mwa Kenya wameamua kuwaita watoto wao jina la Papa Francis,kama heshima kwa ziara ya Papa huyo kulingana na gazeti la The standard nchini humo. ''Ningependa mwanangu kubarikiwa na awe maarufu kama Papa mwenyewe.Ningependa pia yeye aguse maisha ya watu wengi duniani,alisema mmoja ya akina mama walionukuliwa katika habari hiyo''. Hospitali kuu ya Kakamega iliandikisha rekodi ya watoto 13 tangu siku ya jumatano wakati ndege iliombeba Kiongozi huyo wa kanisa katoliki iwasili katika uwanja wa ndege Jomo Kenyatta jijini Nairobi.