Urusi kushirikiana kupambana na IS

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais wa Urusi Vladmir Putin na mwenziye wa Ufaransa Francois Hollande

Urusi imesema iko tayari kushirikiana katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State.

Rais Vladmir Putin amemwambia mweziye wa Ufaransa Francois Hollande, kuwa shambulio dhidi ya ndege ya abiria ya Urusi na lile lililotokea mjini Paris, ambayo yote kundi la Islamic State limekiri kuhusika, kumefanya nchi hizo kuungana dhidi ya adui wao huyo.

Rais huyo wa Ufaransa yupo nchini Urusi kama sehemu ya kujaribu kutafuta muungano kuweza kuwadhibiti wapiganaji wa Islamic state nchini Syria.