Israel kufungua ubalozi milki za kiarabu

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Israel imesema kuwa ina mpango wa kufungua afisi za kibalozi katika milki za kiarabu majuma machache yajayo ingawa mataifa hayo mawili hayana uhusiano rasmi.

Afisi hizo zitakuwa na afisa mmoja wa ubalozi atakayekuwa na chumba katika afisi ya kitengo cha nishati mbadala katika Abu Dhabi, baadala ya kuwa kama ubalozi maalumu wa nchi za milki ya kiarabu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption UAE

Lakini afisa mmoja kutoka wizara ya mashauri ya kigeni amesema kuwa itakuwa mara ya kwanza kwa Israel kufanaya hivyo.

Kumekuwa na biashara za kisiri kati ya Israel na mataifa hayo ya Emirata ,ijapokuwa hakuna ushirikiano rasmi kutokana na mataifa hayo kuiunga mkono Palestina.