Mgombea wa shindano la malkia azuiwa kuingia Uchina

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi Anastasia akizungumza na vyombo vya habari

Mgombea wa mashindano ya malkia wa dunia kutoka Canada amesema kuwa alizuiwa kupanda ndege ya kuelekea Uchina kutoka Hong Kong.

Anastasia Lin mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mzaliwa wa Uchina amesema kuwa hakupata mwaliko kuhudhuria hafla hiyo hatua ambayo ilimzuia kutuma ombi la kupata viza.

Lakini alijaribu kusafiri kuelekea Sanya kupitia Hong Kong,kwa kuwa watalii kutoka Canada hupewa Viza wanapowasili.

Bi Lin amelaumu tukio hilo kwa kampeni zake za kibinaadamu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bi Lin Anastasia

Amekuwa akikosoa 'ukandamizaji na ukaguzi' nchini Uchina na ni mwanachama wa kundi moja la kidini ambalo Uchina inalichukulia kama dhehebu na imelipiga marufuku.

Mashindano hayo ya malkia wa dunia yanatarajiwa kufanyika katika hoteli ya kitalii ya Sanya mnamo terehe 19 mwezi Disemba.

Wakati alipotoa malalimishi yake kwamba hakupewa mwaliko,BBC ilijaribu kuwasiliana na mamlaka ya mashindano hayo lakini haikupata jibu lolote.

Haki miliki ya picha
Image caption Lin Anastasia wa Canada

Magazeti ya Canada The Globe na Mail yaliinukuu taarifa kutoka kwa ubalozi wa Ottawa kwamba Uchina hairuhusu mtu ambaye amepigwa marufuku kungia nchini humo,kufuatia malalamishi ya Bi Lin.