Papa Francis aonya kuhusu ongezeko la joto

Image caption Ziara ya Papa Francis Kenya

Papa Francis amesema ni jambo la aibu kama viongozi wa dunia hawatafikia muafaka juu ya namna ya kupambana na ongezeko la joto duniani.

Akizungumza katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP) mjini Nairobi, Alhamisi kiongozi huyo wa Kanisa katoliki duniani alisema maslahi ya watu fulani hayapaswi kuruhusiwa kutawala badala ya manufaa ya wote.

Kabla ya kuzungumzia hayo Papa Francis alikutana na viongozi wa dini ili kujadili umuhimu wa mazungumzo, na kuwa na misa za wazi kabla kukutana na umati wa maelfu ya waumini katika mji mkuu wa Kenya.

Katika ziara yake barani Afrika, kiongozi mkuu huyo wa Kanisa Katoliki amepangiwa kuelekea nchini Uganda leo na kuimalizia Jamhuri ya Afrika ya Kati Novemba 30.