Uturuki yasema iko tayari kufanya kazi na Urusi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ahmet Davutoglu

Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema kuwa Ankara itafanya kazi na Urusi pamoja na washirika wake ili kuzima wasiwasi baada ya Uturuki kuidungua ndege ya Urusi.

Akiandika katika katika gazeti la the New York Times ,bwana Davutoglu amesisitiza kwamba makabilino dhidi ya Islamic state ndio swala muhimu.

Lakini pia amesema kuwa Uturuki ni sharti itetee uhuru wake.Urusi imesema ndege ya kijeshi ya Uturuki aina ya F-16 iliianguisha ndege yake aina ya SU-24 bombers katika anga ya Syria siku ya Jumanne.

Lakini Uturuki inasema kuwa ndege hiyo ilipita katika anga yake bila ruhusa.

Image caption Ndege ya kijesi

Ndege hiyo ilianguka katika mlima katika eneo linalomilikiwa na waasi karibu na mpaka wa Uturuki.

Mmoja wa rubani wa ndege hiyo alifariki alipomiminiwa risasi wakati alipojaribu kushuka katika ndege hiyo iliokuwa ikichomeka kupitia parachuti.

Rubani mwengine aliokolewa na Urusi pamoja na vikosi maalum vya Syria.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hollande na Putin

Wasiwasi umezuka kati ya Ankara na Moscow kuhusu tukio hilo,huku rais wa Urusi Vladmir Putin akionya kuhusu hatua kali.

Siku ya Alhamisi,alikataa madai ya Uturuki kwamba haikujua kuwa ndege iliodunguliwa ilikuwa ya Urusi.

Bwana Putin alikuwa akizungumza alipokutana na mwenzake wa Ufaransa Francois Hollande mjini Moscow na kuahidi ushirikiano wa karibu dhidi ya Islamic state.