Avunja rekodi ya kutumia taa nyingi katika mti wa Krisimasi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mti wa Krisimasi uliovunja rekodi kwa kuwa wenye taa nyingi zaidi duniani

Mwanamume mmoja kutoka Australia amevunja rekodi ya kutumia mataa mengi zaidi kwenye mti bandia wa Krismasi.

Kitabu cha kuweka rekodi zinazotambuliwa kimataifa cha kampuni ya Guinness World Records, kilithibitsha kuwa Bwana David Richards, alitumia mataa zaidi ya 8,838 kwenye mti mrefu bandia wa chuma ambapo mataa yake yote yalimeremeta.

Mti huo wenye urefu wa mita 22 uliwekwa katika mji wa Canberra.

Watu wa kujitolea kukiwemo mhandisi wa umeme, mhandisi wa ujenzi, wachomeleaji wa vyumba, maseremala, waashi, na watungaji wa vyuma ni baadhi ya watu waliomsaidia katika kampeni hiyo yake ya kuvunja rekodi ya dunia.