Maelfu wahudhuria misa ya Papa Uganda

Image caption Papa Francis akiwa katika ikulu ya Uganda na rais Museveni

Papa Francis amesheherekea misa mbele ya umati mkubwa katika eneo moja takatifu nje ya mji mkuu wa Uganda Kampala.

Mamia ya maelfu ya watu walihudhuria ibada hiyo katika eneo la tukio la mauaji ya wafuasi wengi wa dini ya kikristo mwishoni mwa karne ya 19.

Wakati wa misa hiyo ,Papa Francis aliwaagiza Waganda kutumia mfano wa mashahidi hao kuwakumbusha kuhusu maisha yao ya kila siku kupitia kuwahudumia wazee,masikini na wale waliotorokwa.

Siku ya Jumapili Papa Francis atafanya ziara yake ya mwisho nchini Jamhuri ya Afrika ya kati CAR.