Uturuki yaapa kuwashika waliomuua wakili mashuhuri

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakili Tahir Elci alipigwa risasi jana katika mji wa Kusini Mashariki wa Diyarbakir.

Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutuglu, ameahidi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wauaji wa wakili mashuhuri anayetetea masilahi ya Wakurdi.

Wakili Tahir Elci alipigwa risasi jana katika mji wa Kusini Mashariki wa Diyarbakir.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya watu waliandamana kufuatia mauaji yake

Wakili huyo alikuwa akihutubia mkutana wa wanahabari alipopigwa risasi shingoni akafa.

Afisa mmoja wa polisi pia alifariki katika makabiliano hayo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi walazimika kutibua maandamano ya wafuasi wa Tahir Elci aliyepigwa na kuuawa Diyarbakir

Bwana Elci alipigwa risasi alipokuwa akitoa wito wa amani kati ya wapiganaji Wakurdi wanaotaka kujitenga na maafisa wa usalama

Watu wanaounga mkono makundi ya Kikurdi walisema kuwa mauaji yake yalipangwa kikamilifu.

Haki miliki ya picha hurriyet
Image caption Elci alipigwa risasi alipokuwa akitoa wito wa amani kati ya wapiganaji Wakurdi

Polisi wa Uturuki walitumia mifereji ya maji na kutifua moshi wa kutoa machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji mjini Istanbul waliokuwa wakipinga mauaji ya mwanasheria hiyo.