Ukungu : agizo la kutotoka nje China

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mji wa Beijing umewekwa katika hali ya tahadhari zaidi tangu mwanzo wa mwaka huu.

Utawala nchini Uchina umesema kuwa tahadhari ya uchafuzi wa mazingira iliotolewa katika miji ishirini na tatu siku ya jumapili, itaendelea kudumishwa kwa siku moja zaidi.

Mji wa Beijing umewekwa katika hali ya tahadhari zaidi tangu mwanzo wa mwaka huu.

Viwango vya uchafuzi katika mji mkuu ni mara 17 zaidi ya viwango vinavyo kisiwa kuwa salama na shirika la afya duniani WHO.

Utawala wa nchi hiyo umesema kuwa moshi huo umetokana na mkaa uliotumika majuzi baada ya kuanza kwa msimu wa baridi.

Serikali ya China imetoa amri ya kutotoka nje kwa mamilioni ya watu kwa nia ya kupunguza madhara kwa uma.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Viwango vya uchafuzi katika mji mkuu ni mara 17 zaidi ya viwango vinavyo kisiwa kuwa salama

Zhang Heng ni mkaazi wa Beijing na asema imekuwa vigumu kuishi mjini humo kutokana na hewa chafu.

Ilani hiyo inaamrisha karakana kubwa kupunguza au kuacha kabisa kazi, na imepiga marufuku malori makubwa mabarabarani.

Data iliyokusanywa na ubalozi wa Marekani mjini Beijing, inaonesha kuwa uchafu katika hewa ya mji huo, leo imezidi kiwango kilichowekwa na WHO, kwa mara 20.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ukungu umetanda kote na hata imekuwa shida kuona mbali.

Ukungu umetanda kote na hata imekuwa shida kuona mbali.

Ukungu huo unasababishwa na makaa yanayotumiwa kuleta joto katika majira ya baridi, na kwenye viwanda - na ni tatizo sugu mjini Beijing, na unahatarisha afya wa wanaijiji.