Wasifu wa rais mteule wa Burkina Faso Marc Kabore

Image caption Rais mteule wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kabore

Rais mteule wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kabore ni waziri wa zamani katika utawala wa rais aliyeng'olewa mamlakani Baise Compaore .

Wakati mmoja aliwahi kupigiwa upatu kwamba ndie atakayemrithi .

Hata hivyo yaelekea waburkinabe walimuona kama mwanamme jasiri aliekwenda kinyume na matakwa ya mkubwa wake alipotaka kurefusha muda wake mamlakani .

Roch Marc Christian Kabore ana umri wa miaka 58, alikuwa mfanyikazi wa benki kwa miaka mingi, alihudumu kama waziri mkuu na kushikilia nyadhifa za uwaziri mbalimbali wakati kipindi kirefu cha utawala wa Rais Blaise Compaore.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais aliyeng'olewa mamlakani Baise Compaore

Alikuwa mbunge wa chama cha rais cha Christian Democratic Party( CDP ) kwa zaidi ya miaka kumi.

Alionekana kama rafiki mwaminifu wa kiongozi aliyepinduliwa katika maasi ya wananchi mwaka mmoja uliopita.

Uwepo wake katika upinzani ambacho ni kipindi cha chini ya miaka miwili unaweza kuchukuliwa kama kuendeleza uongozi wa Compaore

Waangalizi wengi wamekubaliana kuwa Kabore aliweza kuwavutia raia wengi wa Burkina Faso kwa kuonyesha ukakamavu wa kumpinga rais wa zamani Campaore kutaka kubadilisha katiba ili kuongoza kwa miaka mingine mitano

Alibuni chama chake alipokiaga chama cha Compaore cha CDP.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Roch Marc aliongoza maandamano akishirikiana na mashirika ya umma kupinga kuongezwa kwa muhula wa tatu wa urais nchini Burkina Faso

Roch Marc aliongoza maandamano akishirikiana na mashirika ya umma kupinga kuongezwa kwa muhula wa tatu wa urais nchini Burkina Faso.

Kwa Rais mteule Kabore lengo lake kubwa kwa miaka mitano ijayo itakuwa kuimarisha demokrasia kwa wananchi wa Burkina Faso na pia kusaidia kusuluhisha maswala ya kijamii na uchumi katika nchi hiyo ambayo imeorodheshwa kama moja ya nchi maskini zaidi ulimwenguni kwa miaka mingi.